Sera za Mpango wa Gmail

Sera za Mpango wa Gmail zinatekeleza jukumu muhimu katika kudumisha hali bora kwa kila anayetumia Gmail. Tafadhali angalia mara kwa mara, kwa sababu sera hizi zinaweza kubadilika. Tafadhali rejelea Sheria na Masharti ya Google kwa maelezo zaidi.

Barua Taka na Barua Pepe Zinazotumwa kwa Wapokeaji Wengi

Usitumie Gmail kusambaza barua taka au barua pepe za biashara ambazo hazijaitishwa na wapokeaji.

Huruhusiwi kutumia Gmail kutuma barua pepe zinazokiuka Sheria ya CAN-SPAM Act au sheria zingine dhidi ya barua taka; kutuma barua pepe ambazo hazijaidhinishwa kupitia seva za wahusika wengine, au zilizo wazi; au kusambaza anwani ya barua pepe ya mtu yeyote bila ruhusa yake.

Huruhusiwi kufanya kiolesura cha Gmail kiweze kufanya yafuatayo kiotomatiki; kutuma, kufuta, au kuchuja barua pepe, kwa namna inayopotosha au kuwahadaa watumiaji.

Tafadhali kumbuka kwamba unachokiita barua pepe “zisizoitishwa” au “zisizotakikana” kinaweza kuwa tofauti na mtazamo wa anayepokea barua pepe zako. Tumia busara unapotuma barua pepe kwa idadi kubwa ya wapokeaji, hata kama wapokeaji hao walichagua kupokea barua pepe kutoka kwako hapo awali. Watumiaji wa Gmail wanapotia barua pepe alama kuonyesha ni barua taka, hili huongeza uwezekano kwamba barua pepe utakazotuma hapo baadaye pia zitachukuliwa kuwa ni barua taka na mifumo yetu inayolinda dhidi ya matumizi mabaya.

Kufungua na Kutumia Akaunti Nyingi za Gmail

Usifungue wala usitumie akaunti nyingi kukiuka sera za Google, kukwepa vizuizi vya akaunti za Gmail, kuepuka vichujio au kubatilisha kwa njia nyingine mipaka iliyowekwa kwenye akaunti yako. (Kwa mfano, kama umezuiwa na mtumiaji mwingine au akaunti yako ya Gmail imefungwa kwa sababu ya matumizi mabaya, usifungue akaunti nyingine ya kufanya shughuli kama hizo.)

Huruhusiwi pia kufungua akaunti za Gmail kwa njia za kiotomatiki wala huruhusiwi kununua, kuuza, kubadilisha au kuuza tena akaunti za Gmail kwa watu wengine.

Programu Hasidi

Usitumie Gmail kusambaza virusi, programu hasidi, vidudu, hitilafu, faili za Trojan, faili zilizovurugika au vitu vingine vyovyote vya uharibifu au udanganyifu. Vilevile, usisambaze maudhui yanayodhuru au kukatiza utendakazi wa mitandao, seva au miundo msingi mingine ya Google au ya wengine.

Ulaghai, Hadaa na Shughuli Zingine za Udanganyifu

Hustahili kufikia akaunti ya Gmail ya mtumiaji mwingine bila ruhusa yake dhahiri. Usitumie Gmail kuwadanganya, kuwapotosha au kuwahadaa watumiaji wengine washiriki maelezo kwa hila.

Usiwahadae watumiaji wengine ili upate maelezo yao ya kibinafsi kama vile maelezo ya kuingia katika akaunti, manenosiri, maelezo ya kifedha au nambari za vitambulisho vya serikali, wala usitumie Gmail kama sehemu ya njama ya kuwalaghai watu wengine.

Usalama wa Watoto

Google ina sera ya kupinga vikali maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa ngono dhidi ya watoto. Tukitambua maudhui kama hayo, tutapiga ripoti kwa shirika la National Center for Missing and Exploited Children kama inavyohitajika kisheria. Tunaweza pia kuchukua hatua za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kufunga Akaunti za Gmail za waliohusika.

Hakimiliki

Fuata sheria za hakimiliki. Usikiuke haki za uvumbuzi za watu wengine, zikiwemo hataza, chapa za biashara, siri za biashara, au miliki bunifu nyingine. Huruhusiwi kuwahimiza au kuwashawishi watu wengine kukiuka haki za uvumbuzi za watu wengine. Unaweza kuripoti ukiukaji wa hakimiliki kwa Google kwa kutumia fomu hii.

Unyanyasaji

Usitumie Gmail kuwanyanyasa, kuwaogofya au kuwatisha watu wengine. Akaunti ya mtu yeyote atakayepatikana akitumia Gmail kwa madhumuni kama haya itafunguwa.

Shughuli zilizo kinyume cha Sheria

Fuata sheria. Usitumie Gmail kuendeleza, kupanga au kushiriki katika shughuli zilizo kinyume cha sheria.