Picha za zamani zinaboreshwa kwa kutumia kichanganuzi kipya zaidi.

Changanua picha haraka zaidi

Usipige tu nakala za picha zako jinsi zilivyo. Boresha picha zilizochanganuliwa kidijitali, ukitumia kipengele cha kutambua pembe za picha kiotomatiki, kipengele cha kurekebisha mwelekeo na kipengele mahiri cha kuzungusha.

Picha maridadi ambazo hazina mweko

PhotoScan huweka pamoja picha nyingi ili kuondoa mweko na kuboresha ubora wa picha ulizochanganua.

Panga picha zako ukitumia programu ya Picha kwenye Google

Hifadhi nakala za picha ulizochanganua kwa kutumia programu ya Picha kwenye Google. Picha zako zitakuwa salama, zitapatikana kwa urahisi na zitapangwa vizuri kulingana na watu na vitu vilivyomo. Pia, huisha picha hizo kwa kutumia filamu, vichujio na vidhibiti vya kina vya kuhariri.

Pata kichanganuzi kipya zaidi cha picha